Loading the content... Loading depends on your connection speed!

Sasa tumefika Bukoba

Benki ya Mkombozi imefungua tawi mkoa wa Kagera, Desemba 15, 2015. Tawi hilo lilizinduliliwa na Askofu wa Jimbo la Bukoba, Mhashamu Desiderius Rwomo.

 

Hii ni fursa kwa wakazi mjini Bukoba na mkoa wa Kagera kwa ujumla kufaidi huduma zinazotolewa na banki hii inayokua kwa kasi.

 

Miongoni mwa fursa hizo ni mikopo ya wajasiriamali wadogo na wakubwa, mikopo ya kampuni, mikopo ya wafanyakazi, ufunguaji wa akaunti za akiba na za muda maalumu.

 

Ni fursa pia kwa wakazi wa Kagera kuimiliki benki hii kwa kununua hisa ili kufaidi gawio la faida kulingana na biashara ya benki hii.

 

Benki ya Mkombozi imeanza kufungua matawi maeneo mbalimbali baada ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuridhika na namna inavyojiendesha na kuinua uchumi wa nchi.

 

Ni Benki iliyoanza kufanya kazi nchini Agosti 28, 2009 ikiwa na tawi moja la St. Joseph lililopo Potsa ya zamani  kitalu namba 40, mtaa wa Mansfield. Tangu kuanza kwake, Benki imekuwa ikifanya kazi kwa ufanisi wa hali ya juu.

 

Mpaka sasa ina matawi  sita  nchini. Matawi mengine yapo Mwanza, Moshi, Msimbazi Centre  na Kariakoo.

 

Kwa kuwa ukuaji wa Benki kwa sasa ni mzuri ni fursa kwa wakazi wa mkoa wa Kagera, kushiriki katika kufurahia matunda ya benki hii kwa kuangalia ni kwa namna gani wanaweza kutumia huduma za kibenki kwa faida yao na uchumi wa Taifa kwa jumla.

 

Benki ya Mkombozi ilianzishwa na Kanisa Katoliki na sasa inamilikiwa na wananchi, kwa mtindo wa kununua hisa, bila kujali imani za dini wala kabila.

24 Responses to Sasa tumefika Bukoba

 1. Revocatus R.Sanka - Reply

  February 11, 2016 at 12:38 pm

  Nimepokea taarifa hizi kwa moyo mkunjufu kabisa kwa sababu mimi ni mmoja wa wanunuzi wa hisa za Benki yetu ya Mkombozi.
  Nimekuwa nje ya Jimbo Kuu la DSM kwa muda mrefu tangu mwaka 2006. Nakumbuka nilinunua hisa 100 kupitia Jimbo la Lindi.Mwaka 2008 nilihamia Bukoba, Januari 2011 nikahamishiwa Mwanza kikazi. Pale Mwanza nilifanikiwa kununua hisa nyingine 100. Tangu Novemba 2013 niko hapa Tabora.Hivyo nina jumla ya hisa 200 kwenye Benki ya Mkombozi.
  Kusema ukweli sijawahi kuhudhuria mikutano yoyote ya Wanahisa na ningependa kujua hatima ya hisa hizo kama kuna maendeleo yoyote.
  Nimefarijika kupata taarifa ya kufunguliwa Benki ya Mkombozi Jimbo la Bukoba.
  Kikazi nipo Natinal Housing Corporation sasa nipo Tabora.

  • Weston Kaluwa - Reply

   February 12, 2016 at 7:12 am

   asante sana ndugu Revocatus, tunakuomba uwasiliane nasi kwa simu zetu za ofisini ulizia kuhusu kupata vyeti vyako vya hisa na jinsi gani unaweza kuja kwenye mkutano mkuu wa wanahisa wote utakaofanyika mwezi wa tano mwaka huu hapa Dar es salaam

 2. France Projest - Reply

  April 8, 2016 at 9:25 am

  Ningependa kujua vigezo vya kuomba mkopo kutoka mkombozi bank kwan wakazi wengi wa bukoba tunashindwa kuomba mikopo sababu hatujui vigezo.asanten sana

  • Weston Kaluwa - Reply

   April 11, 2016 at 10:53 am

   France tembelea moja ya matawi yetu yalio karibu na wewe Tanzania nzima tuko Dar es Salaam, Mwanza, Moshi na Bukoba au piga simu namba 022 2137806/7 ulizia idara ya mikopo upate maelezo ya kina. Karibu sana

 3. Ashery K.Petro - Reply

  April 29, 2016 at 4:19 pm

  Nashukuru kwa kuendeleo kufungua matawi ya benki ya mkombozi,mimi nami ni mwanahisa niliwa kununua mara ya kwanza kabisa mwaka 2006 hisa 200 na cheti nilipata mwaka 2010,juu ya hisa zilizoongezeka.Baada ya hapo tulihamasishwa kuongeza hiza ili kukuza mtaji wa benki hii hapa kigoma Jimboni, ambapo mimi niliweza kuongeza hisa 800.Lakini baada ya hapo sijapewa taarifa yoyete ya mwanahisa hata ile ya kushiriki vikao vya wanahisa tukaambiwa kitu gani kifanyike nasi tukachangia mawazo yetu,labda mnafikiliaje nasi watu wa Kigoma kutuletea tawi ili tuendelee kufaidi matunda ya mkombozi bank?Kwa reference ya kumbukumbu niliyokuwa nimepewa mwanzo ni 2124/06 jina Ashery K.Petro.

  • Weston Kaluwa - Reply

   May 29, 2017 at 6:57 am

   Habari Ashery. asante kwa kuendelea kuwa mwanahisa wa Mkombozi Benki. Kama unafuatilia vema benki yako kila mwaka huwa tunafanya Mkutano Mkuu wa Wanahisa wote (AGM) na katika mkutano huo wanahisa huwa wanajadili hoja mbalimbali na kuzitolea maamuzi. Kwa mwaka huu 2017 Mkutano mkuu umeridhia kila mwanahisa kupata gawio (Dividend) la Tsh. 20 kwa kila hisa moja anayomiliki. Taratibu jinsi ya kulipwa gawio zitatangazwa kupitia vyombo vya habari yaani TV na magazeti na Maparokiani.

 4. Gabriel - Reply

  May 3, 2016 at 8:12 am

  Nashukulu huduma zenu zuri
  .. Mungu awasaidue.
  Shida yangu ni kutaka kujua bei ya hisa moja ni shilingi ngapi kwani naitaji kununua hisa kutoka kwenye benki yenu. Pamoja Na vigezo vinavyohitajika ili kuweza kununua hisa…

  • Weston Kaluwa - Reply

   May 29, 2017 at 6:47 am

   Hello Gabriel,

   Kwasasa bei ya hisa hutegemea hali ya soko la hisa Dar es Salaam (DSE), inaweza kupanda au kushuka. Hisa za Mkombozi Bank kwa sasa zinauzwa kwa Tsh. 1,000 kwa hisa moja. Ili kupata ushauri zaidi temeblea Madalali (Stock Brokers) walio idhinishwa na DSE au tembelea tawi lolote la benki ya Mkombozi na utapewa mwongozo.

 5. Said hassan mswadiko - Reply

  May 8, 2016 at 8:27 am

  Mimi niko karagwe naitaji kujua utaratibu wa kufungua accaunt kwenye tawi lenu
  tell 0786785314
  ahsante

  • Weston Kaluwa - Reply

   May 29, 2017 at 6:50 am

   Bwana Said, karibu sana kwenye tawi letu la Bukoba, Jamhuru Road mkabala na Kituo cha Police au piga simu kwa meneja wa tawi namba 0758 166 734 ili kupata msaada

 6. Alex Muta - Reply

  May 18, 2016 at 9:46 am

  Ni kweli mnataka kufungua tawi Tunduma?

  • Weston Kaluwa - Reply

   May 29, 2017 at 6:52 am

   Ndugu Alex, bado tupo kwenye mchakato wa kufungua matawi mapya na Tunduma ni eneo ambalo pia tuna mpango wa kuweka tawi siku za usoni. Natumaini tutawafikia haraka iwezekanavyo.

   • Elizabeth - Reply

    July 17, 2017 at 12:06 am

    mbona kila nikija kutoa pesa western union naambiwa hakuna network s bora kibao kitolewe

    • Weston Kaluwa - Reply

     July 19, 2017 at 9:44 am

     pole sana Elizabeth, tunaomba radhi kwa usumbufu hii inatokana na kukosa mawasiliano baina yetu na mtandao wa Western Union. Karibu sana utape huduma zote za kibenki katika benki yako ya Mkombozi

 7. rhoda - Reply

  August 18, 2016 at 10:27 am

  nawapongeza sana kwa huduma nzuri, mtu binafsi akitaka kukopa inakubalika

  • Weston Kaluwa - Reply

   May 29, 2017 at 6:37 am

   Habari Rhoda,

   Benki ya Mkombozi inatoa mikopo kwa watu binafsi, vikundi, makampuni na wafanyakazi kupitia mwajiri. Fika tawi lolote la benki upate maelezo ya kina toka kwa wafanyakazi wa benki walio tayari kukuhudumia wakati wowote. Karibu sana.

 8. Medson Oscar - Reply

  September 27, 2016 at 5:19 pm

  Dodoma hakuna taw?i,mi napenda kujua utaratibu wa kujiunga na kuwa mwanahisa.

  • Weston Kaluwa - Reply

   May 29, 2017 at 6:35 am

   Habari bwana Medson,

   Kwa sasa hatuna tawi Dodoma ila bado unaweza kuwa na account na sisi na kuendelea kunufaika na huduma nzuri za Mkombozi Bank. Kwa mikoa ambayo hatuna matawi unaweza kufanya miamala ya kifedha (kuweka fedha kwenye akaunti yako kupitia benki mshirika Benki ya Posta na kutoa hela kupitia ATM za UMOJA SWITCH zilizopo nchi nzima kwenye benki zaidi ya 30)

   Kuhusu suala la kuwa mwanahisa ni rahisi sana, tembelea wakala yoyote wa Soko La Hisa Dar es Salaam (DSE) ili kuweza kununua hisa za Mkombozi Bank au wasiliana na tawi lolote la Mkombozi Benki upate maelezo zaidi

 9. pierre - Reply

  November 1, 2016 at 2:57 pm

  Safi sana tupo pamoja katika kulikomboa taifa letu kiuchumi kupitia benki yetu.

  • Weston Kaluwa - Reply

   May 29, 2017 at 6:29 am

   Asante sana kwa kuwa nasi mdau wetu. Endelea kutumia benki yako ya Mkombozi

 10. samwel Godbless - Reply

  May 27, 2017 at 5:06 am

  Nawezaje kupata mkopo ambapo mimi sio mfanya kazi wa serikali??

  • Weston Kaluwa - Reply

   May 29, 2017 at 6:28 am

   Habari bwana Samwel,

   Tafadhali fika katika tawi lolote la Mkombozi Bank lililo karibu na wewe au wasiliana nasi kwa namba 2137806/7 na utaunganishwa na wahusika upate ufafanuzi zaidi.

 11. Bertha Mbawala - Reply

  June 22, 2017 at 1:31 pm

  Habari za kazi kaka Weston,
  Samahani nilipata taarifa kuwa natakiwa kujaza fomu za gawio, sasa mimi nilikuwa na ombi la kutaka hilo gawio litumike kuongeza hisa zangu zaidi, badala ya kupewa mimi hicho kiasi,kiniongezee hisa

  • Weston Kaluwa - Reply

   June 23, 2017 at 6:45 am

   hello Bertha, unaweza ndio kujaza kwenye hiyo form kama unataka gawio lako litumike kununua na kuongeza hisa zako.

Leave a Comment